Wednesday, 26 March 2014
Monday, 17 March 2014
BABOON
Rooney:''Hili ni jinamizi tupu''
Wayne Rooney
Mshambulizi wa Manchester United Wayne Rooney amesema kuwa kipigo cha mabao 3-0 walichokipata kutoka kwa Liverpool ni kama janga kwake na hiki ndio kipindi kigumu kwake kuwahi kukishuhudia tangu kuanza kucheza soka ya kulipwa.
Steven Gerrard aliingiza mabao mawili kutokana na mikwaju miwili ya Penalti na kukosa la tatu kabla ya Luis Suarez kuongeza bao la tatu.
Mchezaji Nemanja Vidic alifurushwa uwanjani kwa kufanya masihara.
Rooney mzaliwa wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28, amesema kuwa hiki ni kipindi kigumu sana kwake na wembe ambao hautoshi hata kumezwa.
"hili ni jinamizi . Ni siku mbaya sana kwangu , sijawahi kuhisi vibaya hivi maishani mwangu nikicheza soka.
''Yaani hata ni vigumu kutafakari. Liverpool ilicheza vyema sana , lakini hii ni hali ngumu kwangu, '' alisema Rooney
''Hakuna anayetaka kushindwa hapa hasa katika uwanja wa nyumbani, sio vizuri.''
Rooney,aliyesaini mkataba mpya na klabu hiyo, mwezi jana , alipata tu fursa moja ya kujaribu kuingiza bao katika mechi hiyo ambayo Liverpool ilidhibiti tangu mwanzoni ingawa hakufanikiwa
Man U wanashikilia nafasi ya saba katika jedwali la pointi , ingawa Rooney anayepokea mshahara wa pauni laki tatu kwa wiki amesema kuwa hajafa moyo sana kutokana na matokeo mabaya ya Manchester United.
Kocha wa klabu hiyo David Moyes amesema kuwa aliachwa kinywa wazi asijue la kusema.
CHATU AMSHINDA MAMBA
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake
Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC
"Tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumbana mamba hasa katika sehemu ya miguu ili kumdhibiti.''
"Pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kuanza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua nyoka muda wa robo saa kumla mamba huyo.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu saa 5. Hatimaye wote walionekana wachovu.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.



